Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akihutubia leo kwenye mazishi ya Watanzania waliofariki dunia katika ajali ya MV Nyerere yaliyofanyika Mwanza, Ukerewe amesema Serikali ina mpango wa kuunda tume kuu ya uchunguzi itayohusisha wataalamu na vyombo vya dola ili kuchunguza kwa kina kubaini chanzo cha ajali na wote waliohusika kutokea kwa ajali hiyo kuchukuliwa hatua stahiki.

Amesema kuwa tume hiyo itatangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Majaliwa ameongezea kuwa tayari maafisa wote wanaohusika na shughuli za uendeshaji wa kivuko cha MV Nyerere pamoja na wote wenye wajibu wa kusimamia usalama wa kivuko wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano ya awali.

Aidha, Serikali inampango wa kuleta kivuko cha muda wakati taratibu za kuleta kivuko kingine zikiwa zinaendelea.

Rais Magufuli aivunja bodi ya Tamesa kufuatia ajali ya MV Nyerere
Video: Kamwelwe ataja idadi maiti zilizoopolewa

Comments

comments