Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haina mpango wa kununua madeni yaliyosababishwa na mikopo ya kibenki kwenye vyama vikuu vya ushirika nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Julai 7, 2018 wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.

“Serikali ya awamu ya tano hatuna biashara ya kununua madeni ya vyama vikuu, kulikuwa na tabia ya watu wa ushirika kukopa na hali ikiwa mbaya wanakimbilia Serikalini. Serikali hii hatuna biashara hiyo,” amesema.

“Nimeambiwa KCU wamekopa fedha benki ili kulipa deni la mwaka 2014, hii inaingia akilini kweli? Mnakopa fedha kulipa deni la zamani, ni kwa nini msiwatafute waliosababisha deni na kuwachukulia hatua?,” alihoji.

“Ninyi mlikuwa watu sita ambao mlikubaliana kama viongozi, mlienda kukopa kuzidi uwezo mlionao. Leo hii ni kwa nini serikali ije kulipa wakati mmetumia ninyi?,” aliuliza Waziri Mkuu.

Jeshi la Polisi kufanya operesheni kali visiwa vya viwa Viktoria
CUF yatangaza kusitisha kushiriki uchaguzi mdogo wa marudio

Comments

comments