Serikali imetangaza kuwarudisha kazini watumishi 450 kati ya 1,o50 walioondolewa kimakosa  kwenye utumishi wa umma wenye vyeti feki huku ikitoa ufafanuzi kuhusu makosa hayo yaliyotokea.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurian Ndumbaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa rufani za wafanyakazi 600 hazikukubalika.

Amesema kuwa waliorejeshwa kazini walibainika kuwa na vyeti halisi lakini walibadili majina yao baada ya kuolewa, kuchelewa kuchukua vyeti vyao shule walizosoma na kupewa vyeti vilivyofutika, hivyo gamaba kuwa na tatizo laikini matokeo yako sahihi.

“Baada ya kuwahoji na kuwachunguza kwenye shule walizosoma tumebaini ukweli, tumechambua na kuwarudisha kazini kwakuwa wanavigezo vyote vya kuendelea na utumishi wa umma,”amesema Dkt. Ndumbaro

Uhakiki wa vyeti ulifanyika mwanzoni mwa mwaka huu na kubaini watumishi 9,900 ambao walipewa muda wa kukata rufani na sasa watumishi 8800 wanaonekana kuridhika kuondolewa kazini.

Hata hivyo, kuhusu wenye elimu ya darasa la saba, Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa sera ya Menejimenti ya umma toleo la mwaka 1998 inaweka sharti la kiwango cha chini cha elimu kuwezesha mtumishi kuajiriwa katika utumishi wa umma elimu kuwezesha mtumishi kuajiriwa katika utumishi wa umma.

Abdelhak Nouri Huenda Asicheze Tena Soka
Pep Guardiola Ampata Mbadala Wa Dani Alves