Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ametoa ufafanuzi mbele ya Bunge kuhusu shilingi Trilioni 1.5 zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali na kusema kuwa zimetokana na matumizi ya dhamana na hati ya fungani zilizoiva ambazo ni shilingi Trilioni 0.6873.

Kijaji ameongezea kuwa Fedha nyingine ni mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar ambayo ni shilingi trilioni 0.2039, kwa mchanganuo huo unafanya jumla ya shilingi Trilioni 1.5891.

Aidha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kuapisha majaji iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es salaam amefunguka na kusema katika ripoti ambayo alipokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad haikuwa na upotevu wa hizo fedha na kusema kama ungekuwepo angechukua hatua kali kwa wahusika siku hiyo hiyo.

Aidha CAG mbele ya mkuu wa nchi amethibitisha hakuna upotevu wowote wa kiasi hiko cha fedha mara baada ya kuulizwa na kuambiwa athibitishie Umma juu ya swala hilo.

 

Bunge kumhoji Mugabe kuhusu utata upotevu mabilioni ya Almasi
EXCLUSIVE: Ukimkuta Mume/mke wako ana 'KISIMBUSI' utafanyaje? | Penyenye (S02E01)