Serikali imesema matumizi ya Teknolojia ya Habari ya Mawasiliano (TEHAMA) hususani kompyuta yanazidi kukua kwa kasi kubwa duniani na hapa nchini, aidha shughuli nyingi za uendeshaji wa ofisi za Serikali na na sekta binafsi, kama vile kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano ya kuhifadhi nyaraka zinafanywa na TEHAMA.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa udhibiti wa huduma za serikali mtandao, Michael Moshiro alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo, amesema kuwa, pamoja na Serikali kubwa ambayo Serikali imeipata katika matumizi ya TEHAMA kwa kipndi kirefu, bado kulikuwa na changamoto ambazo zilikwamisha malengo yaliyokusudiwa kwa haraka.
Aidha, Moshiro amezitaja changamoto hizo ni pamoja na utengezaji au ununuzi wa mifumo ya TEHAMA isiyozingatia mahitaji ya taasisi na serikali kwa ujumla, mifumo isiyoweza kubadilisha taarifa,uwepo wa urudufu wa mifumo na taarifa zinazohifadhiwa na mifumo mbalimbali na rasilimali za TEHAMA yasiyoshirikishi.
Hata hivyo amesema changamoto hizo zilipelekea serikali kutengeneza miongozo na viwango dhabiti itakayowezesha serikali kukabiliana nazo,na kuongeza kuwa serikali ina lengo la kusaidia matumizi ya TEHAMA kwa usahihi