Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema kuwa haijakatazwa mtu kumiliki zaidi ya kadi moja za simu ilimradi ziwe za mitandao tofauti, ambapo amesema kuwa wanatamani kila Mtanzania awe na Line moja ya simu kwa mtandao mmoja akitaka nyingine atoe taarifa.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu kwenye kikao cha Bunge la 11 kinachoendelea, ambapo amesema kuwa lengo kuu ni kupunguza wingi wa kadi hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia vitendo vya uhalifu wa simu ikiwa ni pamoja na wizi akitolea mfano mbinu ya “ile pesa nitumie kwa namba hii.”

”Tunatamani kila Mtanzania awe na Line moja kwa kila mtandao ili kama akihitaji nyingine basi atoe taarifa ili aweze kupatiwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa,”amesema Nditiye

Video: Kangi Lugola awataja wenye sifa za kusajili Laini za simu
Diamond afunguka kisa kuwatelekeza watoto wake Afrika Kusini, "Mwenzangu hataki"

Comments

comments