Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala bora imeamua kuwarejesha kazini watumishi wote waliokuwa wameajiriwa kabla ya Mei 2004 na kuamuru walipwe mishahara yao yote katika kipindi ambacho hawakuwa kazini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa wizara hiyo, George H. Mkuchika wakati akito kauli ya serikali Bungeni katika mkutano wa 11 kikao cha tano cha Bunge la 11, ambapo amesema kuwa serikali imefanya hivyo kutokana na maoni mbalimbali yaliyotolewa na wabunge katika Bunge linaloendelea Mjini Dodoma.

“Serikali imeamua na kuagiza kwamba watumishi wote ambao walikuwa na ajira ya kudumu au mikataba ambapo walikuwa kazini kabla ya Mei 20, 2004 warejeshwe kazini mara moja na walipwe mishahara yao yote kwa kipindi walichokuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao mpaka pale watakapo staafu kwa mujibu wa sheria,”amesema Mkuchika

 

Waziri Mkuu awataka mabalozi kutangaza vivutio vya uwekezaji nchini
Herry Kane apania kumshinda Salah.