Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa wametengua nafasi ya Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Joketi Mwogelo kwa kufuata kanuni za Katiba ya Umoja huo.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa Umoja huo unaongozwa na Katiba hivyo maamuzi yoyote yanayotolewa hufuata taratibu na misingi ya Katiba.

“Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM) daima huongozwa na Katiba, kwa hiyo maamuzi yote yanayofanyika huwa vikao vimekaa kwa kufuata taratibu zote na kuweza kutoa maamuzi,”amesema Shaka

 

Ndugu zangu siwaoni, sijui wametekwa- Hashim Rungwe
Video: Mbowe kizimbani kwa kosa la uasi, JPM alivyoandika barua 25 kwa JK

Comments

comments