Miaka ya hivi karibuni maumbo makubwa yamekuwa yakipaparukiwa na kuonekana ni maumbo yenye mvuto mkubwa zaidi hasa kwa wadada, hali iliyopelekea wanawake wengi wenye uhitaji wa maumbo hayo kuamua kutumia gharama yeyote ile kupata muonekano huo.

Wapo wenye maumbo madogo wanaotaka kuwa na maumbo makubwa vivyo hivyo wapo wenye maumbo makubwa wanaotaka kuongeza zaidi ya kile walichonacho, na pia wapo wenye maumbo makubwa wanaotaka kupunguza ukubwa wa maumbo hiyo.

Teknolojia imekuwa zaidi, madaktari wamevumbua mbinu mbadala ya kuongeza na kupunguza maumbo na kuwa unavyotaka kwa kufanya upasuaji maalum kitaalamu unajulikana kama Plastic Surgery.

Leo katika kipindi cha Zaidi nimekuandalia watu maarufu duniani waliotumia pesa nyingi kubadilisha muonekano wa maumbo yao kwa kufanya upasuaji yaani Plastic Surgery.

Na ifahamike kuwa upasuaji huu unafanyika sio tu kwa wanawake bali hata kwa wanaume ambao nao hupendelea kuongeza au kupunguza sehemu fulani za miili yao.

Tazama na wafahamu wasanii na watangazji hawa maarufu waliowahi kufanya plastic Surgery kurekebisha mionekano ya miili yao hapa.

Live: Kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini
Mwili wa mtoto watelekezwa dampo Iringa