Klabu ya Simba yenye maskani yake mitaa ya msimbazi jijini Dar es salaam imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la ngao ya hisani.

Aidha, katika mchezo huo uliowakutanisha watani wa jadi vilabu vya Simba na Yanga ulivuta hisia za wengi, huku mashabiki wa timu hizo wakitambiana kila mmoja akivutia upande wake.

Timu hizo zilikuwa zikishambuliana kwa zamu huku kila timu ikiimarisha ngome yake ya ulinzi, hivyo kupelekea kumalizika kwa kipindi cha kwanza kutoka uwanjani bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitaka kupata goli la kuongoza ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa kombe hilo, lakini mpaka kipyenga cha mwisho cha mwamuzi kinapulizwa kuashilia kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo,hakukuwa na timu yeyote ambayo ilikuwa imeliona lango la mwenzie, hali ilyopelekea kufikia hatua ya penati ambapo Klabu ya Simba iliibuka kidedea kwa penati 5 dhidi ya Yanga ambayo ilipata penati 4


Magazeti ya Tanzania leo Agosti 24, 2017
Sianga ataja mikakati 3 anayotumia kupambana na dawa za kulevya