Mbunge wa Jimbo la Kibakwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), George Simbachawene amesema kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli hajafanya kosa kuupatia hadhi ya Jiji mkoa wa Dodoma.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa rais ana haki ya kisheria kufanya hivyo.

Amesema kuwa maamuzi aliyoyachukua rais Dkt. Magufuli ni sahihi na wala hayahitaji kuhojiwa na mtu yeyote kwani kisheria na taratibu yuko sahihi.

“Haya maamuzi yako sahihi, rais ana uwezo wa kusikiliza ushauri wa mtu yeyote ama la yeye anachoangalia ni maslahi ya nchi,”amesema Simbachawene

 

Hamisa, Diamond bega kwa bega wafuturisha yatima
CCM yasema haitambui ujio wa Lembeli