Kufuatia tukio la mtoto Pendo Frank “Welu” mwenye umri wa miaka 6 mwenyeji wa Arusha na mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Levolosi, kuripotiwa kupotea siku ya Ijumaa Machi 10, 2017 na kupatikana siku ya Jumatatu, Neema Richard ambaye ni mama mdogo wa mtoto huyo amesimulia tukio la kupotea kwa mtoto huyo na jinsi alivyopatikana.

Neema ametoa simulizi hiyo wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo ameeleza jinsi mtoto huyo alivyopotea na kupatikana huku akiwaasa wazazi kuwa makini na watoto wao ili kuepusha tatizo hilo la upoteaji wa watoto linaloonekana kutokea mara kwa mara katika jamii.

Pamoja na hayo, Neema amewashukuru wote walioshiriki kuhakikisha Pendo anapatikana. Bofya hapa kufuatilia tukio hilo.

Controversial Matters for Research Paper
Chelsea Yaiponza Man Utd, Yatuhumiwa Kufanya Vurugu