Makalio makubwa, hips kubwa na shepu kubwa ndiyo habari ya mjini kwa sasa, muonekano huo unapendwa na watu wengi zaidi na kwa kuwa wadada warembo hugharamia chochote kuhakikisha wanapendeza na kwenda na wakati, ujio wa chupi zenye vigodoro umeongeza thamani ya kile wanachotaka miili yao kuonekana.

Chupi zenye vigodoro ni chupi ambazo humsaidia mwanamke kuoneakana na umbo zuri lenye ujazo wa kutosha kuanzia makalio, hips hadi sehemu ya mbele ya mwanamke.

Wafanyabiashara soko kubwa la Dar es salaam, Kariakoo wamefunguka undani wa biashara ya uuzaji wa chupi zenye vigodoro na kusema kuwa kwa sasa biashara hiyo imepamba moto na wanaoongoza kwa kutumia bidhaa hiyo ni watu wenye rika zote sio tuu kina dada wenye umri mdogo kama ambavyo wengi wanadhani.

”Sio siri tena, zamani tulikuwa tunauza kwa kificho” amesema mmoja ya wafanyabiashara wa vigodoro.

Ile dhana ya kuchoma sindano na kutumia vidonge inakufa siku hadi siku kutokana na ubunifu mkubwa unaofanywa na wataalamu wa urembo, na hii ni kutokana na madhara makubwa yanayotokana na matumizi ya vitu hivyo kama vile kansa.

Sababu mbailimbali zatajwa biashara hiyo kupamba moto miaka ya hivi sasa.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 11, 2019
Video: Makamu wa Rais aongoza kikao cha kujadili masuala ya Muungano

Comments

comments