Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa amesema kuwa hawezi kustaafu uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapomchukua.

Ameyasema hayo Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati wa kukabidhi nyumba 10 za watumishi wa afya zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Wiliam Mkapa, ameema kuwa yeye amestaafu nafasi ya Rais lakini sio uanachama.

“Mimi sijastaafu uanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, bali ni nafasi moja tu ambayo nimestaafu ambayo ni nafasi ya Rais, nitaendelea kuwa mwanachama wa chama changu na kukisaidia mambo mbalimbali,”amesema Mkapa.

Aidha, akizungumza kuhusu sherehe ya makabidhiano ya nyumba hamsini zilizojengwa katika mikoa ya Geita, Simiyu, na Kagera, amesema kuwa ameridhishwa na ushirikiano wa Serikali na Taasisi ya Benjamin William Mkapa katika ujenzi wa nyumba hizo kwani lengo kubwa ni kufikia malengo ya milenia ya 2020

Halmashauri zatengewa fedha za dawa kila mwezi
Balozi wa Everton asifu ukarimu wa Watanzania