Rapa Solo Thang anayeishi ugaibuni hivi sasa amemtetea Jay Mo baada ya kukosolewa na baadhi ya wasanii na wadau wa muziki nchini kuhusu  mabadiliko na ujio wake mpya wa ‘Pesa ya Madafu’.

Baadhi ya wadau wa muziki walikosoa mabadiliko ya mtindo wa kuchana aliokuja nao Jay Mo kwenye wimbo huo, wakidai kuwa ameiacha ‘hip hop’ halisi iliyompa mashabiki wengi waliokuwa wakisubiri ujio wake.
“All this nonsense of what Trap beat, Dab and Stuff,, you can’t take #HipHop out of JaY Moe,, He is #HipHop,#PesayaMadafu  is a hit, Period.” Inasomeka tweet ya Solo Thang ambaye anajipanga kuachia albam yake mpya aliyoibatiza jina la ‘S.U.MU.

Jay Mo alikamilisha video ya ‘Pesa ya Madafu’ nchini Afrika Kusini na amekuwa akisisitiza kuwa ujio wake mpya hauna mtazamo wa kutaka kushindana na wasanii wanaofanya vizuri hivi sasa bali kuwarudia mashabiki wake.

John Legend amchana Donald Trump ‘kivyake’
Ronaldo Aonyesha Dharau Dhidi Ya Iceland, Mashabiki Wamshambulia