Kampuni ya usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment imepigwa faini ya shilingi milioni 7 kwa uchafuzi wa mazingira na imetakiwa kulipa faini hiyo kwa muda wa siku 7.

Kampuni hiyo imetozwa faini kufuatia oparesheni  ya ukaguzi wa mazingira na viwanda jijini Dar Es Salaam inayofanywa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina ambapo alitembelea kiwanda cha kutengenezea CD, tape na DVD cha Steps Entertainment na kujionea uchafuzi wa mazingira kwa kutiririsha maji ya chooni katika mfereji wa maji ya mvua wa Airport. Bofya hapa kutazama video  #USIPITWE

Manispaa Morogoro yapewa siku moja kutenga maeneo ya Wafanyabiashara wadogo
Video: Romelo Lukaku Amkataa Martinez Kwa Hisia