Msanii wa maigizo ya vichekesho Steve Nyerere amezungumza na vyombo vya habari leo juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili na kukanusha kuwa hakukurupuka kwa kile alichokuwa anafanya kipindi cha msiba wa mtoto wa msanii mwenzake Muna.

Siku ya jana Muna alizungumza na vyombo vya habari na kusema Steve Nyerere alikuwa anafanya mambo bila kushirikiana naye akiwa Nairobi, na kusema yote yalifanyika ilikuwa ni mipango ya aliyekuwa mume wake Peter Zacharia.

Msikilize Steve akizungumza na vyombo vya habari akimjibu Muna Love

Peter Zacharia ambaye ni mume wa ndoa wa Muna love, licha ya kuwa waliachana na mwanaume huyo miaka mitano iliyopita kwa kisa ambacho hakutaka kukitaja akidai kuwa ataidhalilisha familia yake.

Umaarufu wa Peter umekuja mara baada ya kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai kuwa Patrick ni mtoto wake aliyemzaa kwenye ndoa ila siku ya jana Muna aliweka wazi na kusema kuwa marehemu Patrick ni mtoto wa Casto Dickson aliyemkataa pindi akiwa na mimba ya wiki mbili.

Aidha watu mbalimbali wameibuka wakiwemo wasanii wenzake ambao wamepinga vikali kitendo cha Muna kuongea na vyombo vya habari kabla hata ya arobaini ya mtoto wake kujafika, wengi wamedai kuwa amewadhalilisha wanawake wenzie.

Muna siku ya jana alisema anaaamini kuwa Mungu amaeamua kumchukua Patrick ili amjaribu imani yake na kamwe hawezi kurudi nyuma.

Aliemuonyesha kadi nyekundu Zidane aeleza alivyopata tabu kutoa maamuzi
Patrick Aussems kocha mpya Simba SC

Comments

comments