Tuzo za 20 za VGMA (Vodafone Ghana Music Awards) zilizofanyika usiku wa Jumamosi Mei 18, 2019 nchini Ghana zilizua taharuki baada ya kuibuka mzozo kutokana na ugawaji tuzo kushidwa kumtangaza mshindi wa kipengele cha msanii bora wa mwaka.

Stonebwoy aliyetangazwa kwa mara tano mfululizo sasa kama mshindi wa kipengele cha msanii bora wa muziki wa Reggae/Dancehall.

Hata hivyo inaonekana muimbaji mwenzake Shatta Wale hakuridhishwa na matokeo yale na kuamua kuivamia stage na kuanza kufanya vurugu kitendo kilichomfanya Stonebwoy kuchomoa bastola jukwaani.

Inaeleza kuwa sababu ya vurugu hiyo ni kwamba wawili hao wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu.

Hata hivyo chanzo cha bifu lao hakijatajwa imeripotiwa kuwa polisi wanamshikilia mwanamuziki Stonebwoy kwa kitendo cha kutoa bastola jukwaani na kuhatarisha usalama wa raia waliokusanyika japo hakuna aliye jeruhiwa.

Serikali yakamilisha upanuzi wa chuo cha Patandi
Mtaelewa tu fitina anazofanya Masele- Spika Ndugai