Mkurugenzi wa Mahusiano Kliniki Dkt. Myrose Majinga amesema kuwa watu wengi wameingia katika mifarakano ya mahusiano na kupelekea kupoteza kazi, Mahusiano ya ndoa na hata udungu, ameeleza lengo kuanzisha kliniki hiyo ni kusaidia watu walioathirika na msongo wa mawazo.

Amesema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media leo Septemba 13, 2021 Katika uzinduzi wa Kliniki hiyo ambapo ameeleza dhamira ya mafunzo hayo ni kuandaa wataalamu watakao kuwa matabibu wa jamii katika kuonesha njia ya mambo yanayoikumba jamii na familia.

”Watu wanamambo mengi ndani hawana mahali pa kuyapeleka tukaona tuanzishe kliniki ya mahusiano ili tusitoe tu ushauri kama ilivyozoeleka, watu wengi wanaogopa kwenda kwa watu kwasababu wanogopa mambo yao ya ndani kuyakuta nje sisi kwetu tunafanya shughuli zetu kama unavyoenda kwenye hospitali yoyote” amesema dkt. Majinga


 

Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) yapigwa msasa
Biteko: usalama ni jambo muhimu katika maeneo ya kazi