Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Fredrick Sumaye amesema kuwa kushindikana kupokelewa kwa Wema Sepetu na kukabidhiwa kadi ya chama hicho kumesababishwa na kesi inayomkabili.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa taarifa za kukabidhiwa kadi kwa msanii huyo itatolewa pale mambo yatakapo enda vizuri.

“Leo tulikuwa tumejiandaa kumpokea na kumkabidhi kadi ili awe mwanachama wetu kamili, lakini kesi inayomkabili ndiyo imesababisha kuahirisha kwa shughuli hii, hivyo tutawajulisha pale mambo yatakapokamilika”.amesema Sumaye

Video: Nimedhamiria kuboresha mazingira ya elimu-Makonda
Taasisi za umma zabanwa kuhusu matumizi ya kuni