Loe Oktoba 7, 2016 Madaktari wametoa majibu juu ya uchunguzi wa macho ya Said maaarufu kwa jina la Baba D ambaye alipata mkasa wa kushambuliwa na kibaka anayefahamika kwa jina la Scorpion, kisha kutobolewa macho yote mawili hali iliyopelekea kutoona.

Serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda imefanya juhudi za kumfikisha Hospitali ya Muhimbili kijana Said ambako alifanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua kama kuna uwezekano wowote wa kumrejeshea uwezo wa kuona lakini juhudi hizo zimeshindikana baada ya madaktari kufanya uchunguzi na kugundua kuwa kijana huyo hawezi kuona tena.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa, Paul Makonda amesema Said alipelekwa hospitali kwa siku mbili mfululizo na kufanyia uchunguzi na madaktari bingwa wa kichwa, mishipa, jicho na mboni ambapo wamefanya jitihada kubwa kuhakikisha anaona tena lakini majibu siyo mazuri na hakuna namna tena ya Saidi kuona tena kutokana na kitendo alichofanyiwa. Bofya hapa kutazama video

Video: Ahadi za Makonda kwa kijana aliyetobolewa macho baada ya majibu ya Hospitali
Best Essay Writers from our Essay Writing Service