Taasisi ya Mgunduzi wa Madini aina ya Tanzanite nchini, imesema kuwa inafanya jitihada ya kuyatangaza madini aina Tanzanite kimataifa ili yaweze kuinufaisha nchi kiuchumi na kimaendeleo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Asha Jumanne Ngoma alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kwasasa taasisi hiyo inafanyakazi ya kuyatangaza madini aina ya Tanzanite ili yaweze kuinufaisha nchi.

Amesema kuwa pamoja na kuyatangaza madini hayo. pia taasisi hiyo inajishughulisha na shughuli za kimaendeleo katika jamii yote iliyozungukwa na aina mbalimbali za madini hapa nchini, kutoa elimu namna ya matumizi ya madini hayo.

”Tumeamua kufanya shughuli hii kwa ajili ya kumuenzi mgunduzi wa madini haya ya Tanzanite, kwasababu alikuwa na moyo wa kipekee na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yake, basi na sisi kwakuwa haya ni matunda ya uzalendo wake, na sisi tumeamua kuendeleza uzalendo huo kwa kuyatangaza madini haya kimataifa kwani yanapatikana Tanzania pekee,”amesema Ngoma

Aidha, katika mkutano wa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini nchini, ulioandaliwa na wizara ya madini, wadau mbalimbali wa sekta ya madini walikutana na kuweza kujadili changamoto zinazowakabili katika sekta hiyo.

Halmashauri ya Mji Njombe yaipiga msasa Manispaa ya Sumbawanga
Makala: Mfahamu Oliver Mtukudzi, Sauti ya Afrika iliyookoa mamilioni