Peter Mollel maarufu kwa jina la ‘Pierre Liqud’ amekabidhiwa tiketi ya usafiri wa ndege ya kwenda na kurudi nchini Misri kushuhudia michuano ya kombe la Mataifa Huru Barani Afrika (AFCON).

Pierre ambaye ni fundi seremala amekabidhiwa tiketi hiyo leo Juni 19, 2019 na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza katika eneo la Bunge jijini Dodoma.

Tiketi hiyo imedhaminiwa na Mradi wa Utambuzi wa wasanii wa Sanaa za Ufundi (TACIP) na tayari Pierre ameshasajiliwa katika mradi huo.

.

 

Vigogo TRA wasukumwa ndani kwa tuhuma ya kuomba rushwa
Wananchi watakiwa kuunga mkono juhudi za Serikali.