Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa tahadhari iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini isipuuzwe.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Itikadi na Uenezi wa Mambo na Nje, John Mrema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa taarifa kama hizo hazipaswi kupuuzwa.

Amesema kuwa Marekani imekuwa ikitoa taarifa mbalimbali katika balozi zake duniani kote ili kuweza kuwalinda raia wake.

”Lengo kubwa la Marekani ni kuwalinda raia wake, ukiangalia tukio la mashambulizi kama lililotokea London, Ufaransa, New Zealand hata hapo kwa majirani zetu Kenya, Wamarekani walitoa taarifa, na kweli mashambulio ya kigaidi yaliyotokea, ombi letu taarifa hizi zisipuuzwe,”amesema Mrema

Hata hivyo, Mrema ameongeza kuwa taarifa kama hizo za kiusalama, hazitakiwi kutolewa kwa kificho bali zinatakiwa kutolewa hadharani ili hatua stahiki zichukuliwe.

LIVE: Yanayojiri Bungeni jijini Dodoma
Kamoli aishukuru serikali kwa kutekeleza miradi yake