Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema Taifa limekosa ubunifu na juhudi za kufanya kazi badala yake watu wamekuwa wakiwaza mishahara kutokana na mfumo katika sekta ya elimu.

Makonda amesema hayo leo Oktoba 22, 2016 wakati akihutubia katika Mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya ST. Joseph Millenium iliyopo Goba jijini Dar es salaam.

Amesema pamoja na kuwa na madini, gesi na vyanzo vingine ambavyo Mungu ameibariki Tanzania lakini wamekosekana wataalamu wa sekta hizo hali inayofanya kuwepo kwa watu wanaokuja na kutumia benki za Tanzania, wanapata mikopo kutoka katika benki hizo huku watanzania wakibakia kama madalali katika nchi yao. Bofya hapa kutazama video

 

Video: Wanafunzi(ST. Joseph) wavyoimba Unconditionally Bae ya Sauti Sol na Alikiba

 

Kama ilikupita hii taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Poul Makonda kuhusu Mfalme wa Morocco, Mohamed VI kutua Dar na ndege sita kubwa na nyingine mbili

Makonda aahidi mifuko 1000 ya cement, magodoro 400 Shule ya St. Joseph Millenium
Maalim Seif aona dalili za pingu mikononi mwake, 'SUK sio ya kuchezea’