Waziri MKuu, Kassim Majaliwa ameagiza apatiwe orodha ya wadaiwa sugu wa taasisi zote za Serikali mkoani Dodoma ambao wamelimbikiza deni la sh. bilioni 1.4 zikiwa ni bili zao za maji.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 2, 2016) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) mara baada ya kukagua utendaji kazi wa chanzo cha maji cha Mzakwe nje kidogo ya mji wa Dodoma.

“Niletee haraka orodha ya wadaiwa wote wa Ofisi za Serikali na taasisi za umma ambao hawajalipa bili zao. Madeni yote ni lazima yalipwe,” – Waziri Mkuu. Bofya hapa kutazama video

Di Matteo Afungasha Virago Na Kuondoka Villa Park
Rigobert Song Yu Hoi, Akimbizwa Hospitali