Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, (TAMWA) wamepongeza hatua zilizochuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda za kuwashughulikia wale wote waliotelekeza familia zao.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Chama hicho, Eda Sanga alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa ni siku nyingi sana chama hicho kimekuwa kikipigania haki za wanawake.

Amesema kuwa TAMWA inaunga mkono kazi inayofanywa na Makonda kwani kufanya hivyo kutasaidia wanawake wengi waliotelekezwa kupata haki zao.

“Ni siku nyingi sana TAMWA tumekuwa tukipigania haki za wanawake waliotelekezwa na watoto, lakini anachokifanya Makonda kitasaidia wanawake wengi waliotelekezwa kupata haki zao na sisi tunamuunga mkono,”amesema Sanga

Video: Sakata la Makonda laanza kuzaa matunda, mmoja akamatwa
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 13, 2018

Comments

comments