Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa tatizo kila anapojaribu  kufanya mawasiliano na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif hapokei simu zake wala simu za wajumbe wa Bodi ya Wadhamini Bara hali ambayo inaendeleza kutoelewana ndani ya chama.

Lipumba amesema yeye ni mwenyekiti halali wa chama hicho kwani alitengua barua yake ya kujiuzulu kabla barua hiyo haijafika katika mkutano mkuu wa chama na alimwandikia barua ya kuanza kazi Katibu mkuu ambaye hakurudisha jibu tena kwake wala kupokea simu zake

Akizungumzia sakata la Maalim Seif kuzuiwa kufanya mkutano wa ndani Mtwara, Lipumba amesema anayepanga mikutano yote ya CUF Bara ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, hivyo Maalim alivyoenda Mtwara alienda bila kutoa taarifa kwa uongozi wa Mtwara hali iliyopelekea mkutano wake kuzuiwa na wananchama wa CUF Mtwara.

Video: Makonda awataka watumishi kubandika majukumu yao kwenye mbao za matangazo ya ofisi
Video: Siri nzito kikao cha JPM, Lukuvi, Serikali yashtuka...