Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa baada ya bunge la bajeti atakuwa na vikao vingi na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na sanaa.

Amesema kuwa analazimika kufanya hivyo ili kuweza kuiokoa tasnia ya filamu nchini ambayo imekuwa ikisuasua kila mara.

Aidha, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Tanzania ina vipaji vingi ambavyo vinaweza kuitangaza na kuliingizia kipato taifa ambacho kitatokana na sanaa.

“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na vipaji vingi sana, lakini kila kukicha vinazidi kupotea, baada ya bunge la bajeti nitafanya vikao vingi ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa matatizo,”amesema Dkt. Mwakyembe

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 18, 2018
Jafo atoa maagizo mazito kwa wakuu wa mikoa

Comments

comments