Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Diamond Platinumz ameachia ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la ‘Iyena’ aliyomshirikisha msanii wake Rayvany.

Ambapo katika video ya wimbo huo aliyekuwa mpenzi wake Zarina Hassan ameonekana akifunga ndoa na Diamond.

Aidha, katika siku za nyuma kwenye mahojiano mbalimbali Diamond Platinumz amewahi kuzungumza juu ya wimbo huo ambapo alisikika akijinadi kuwa tayari ametengeneza wimbo mzuri utakaovuma na kutumika katika maharusi mbalimbali.

Natumaini ndoto yake imetimia kama ilivyo kwa msanii huyo kutokosea hasa pale anapofanya kazi zake, wimbo ni mzuri unachangamsha na utafaa kupigwa katika maharusi mbalimbali.

Aidha uwepo wa Zarina Hassan katika video hiyo unaweza kuleta mtafaruko juu ya mahusiano ya wawili hao ambao walibwagana miezi mitatu iliyopita.

Hata hivyo siku chache zilizopita yalizuka maneno yakidai kuwa Diamond alimpigia magoti Zari kumuomba msamaha ili warudishe penzi lao ila Diamond alipinga tetesi hizo na kudai kuwa alikwenda nchini Afrika Kusini kuwasilimia watoto wake na kuwa yeye na Zari watabaki kuwa wazazi na si vinginevyo.

Bonyeza kitufe chekundu hapa chini kuutazama wimbo wa Iyena.

Mahakama ya Uswiz yamtoa kifungoni Paolo Guerrero
Bahati ya mtende yamuokoa Granit Xhaka