Leo Novemba, 14, 2016 limetokea tetemeko lenye ukubwa wa Richa 6.3 huko New Zealand ikiwa ni muda mchache baada ya kutokea tetemeko lenye mgandamizo wa Tsunam na ukubwa wa Richa 7.8 nchini humo na kuua watu wawili.

Waziri Mkuu wa New Zealand, John Key amethibitisha kutokea kwa matetemeko hayo na vifo vilivyotokea, huku idara ya majanga nchini humo ikiwataka raia wake kuhamia maeneo ya juu ili kujikinga na madhara yatakayotokea na bado wanafanya uchunguzi kujua madhara ya kibinadamu na miundombinu yaliyotokea.

Nchi ya New Zealand imetajwa kuwa na eneo lenye mgandamizo mkubwa wa miamba ambayo hukatika au kupasuka kutokana na kuwa karibu na bahari ya Pacific Ocean ambayo hukumbwa na vimbunga vya Tsunami na iliwahi kupigwa na tetemeko kubwa mwaka 2011 katika eneo la Christchurch na kuua watu 185.

Fid atoa ushahidi jinsi ‘Mdosi’ alivyomuibia mauzo ya albam yake
Memphis Depay: Sifahamu Chochote Kuhusu Mustakabali Wangu