Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema kuwa madhara yanayowakumba wanawake wanaojichubua kwa vipodozi mbalimbali kuwa ni hatari zaidi kwani wengi wao hupatwa na magonjwa ya kansa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Agnes Kijo alipokuwa akizungumza na Dar24 Media,a mbapo amesema kuwa mamlaka hiyo imeanzisha Kampeni mashuleni kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu madhara ya kujichubua.

“Kazi yetu kubwa kwasasa tumeanzisha Kampeni katika mashule mbalimbali nchini ili kuweza kuokoa kizazi hiki, kwani elimu ikitolewa mapema tutaweza kunusuru na matumizi ya vipodozi hivyo,”amesema Kijo

Magazeti ya Tanzania leo Februari 8, 2018
Video: Chadema yalalama kuonewa