Shirikisho la mpira miguu tanzania TFF limejitokeza mbele ya Waandishi wa habari kupitia Afisa habari na mawasiliano, Alfred Lucas na kueleza kuridhia uchaguzi wa klabu ya yanga kufanyika juni 11 kama ilivyokuwa imepangwa na klabu hiyo  na kusimamiwa na kamati ya uchaguzi  yanga chini ya uangalizi wa kamati ya uchaguzi ya TFF.

Awali uchaguzi wa yanga ulipangwa na TFF kufanyika tarehe 25 juni  kutokana na yanga kuchelewa kutangaza tarehe yao ya uchaguzi.

Rais wa TFF Jamali Malinzi amewataka pia wagombea waliochukua fomu za uchaguzi wa yanga TFF nao washirikishwe katika uchaguzi huo pia amewatakia kila kheri katika uchaguzi huo.

Kuna mambo mengine matatu kutoka TFF, Bofya video hapa kuyafahamu

Chadema waambulia Mabomu Kahama, Polisi yapiga marufuku mkutano
Majaliwa: Mpango wa pili wa maendeleo unalenga kuboresha maisha ya maskini