Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania(TFF) limetoa ufafanuzi suala la ratiba ya ligi kuu nchini  na kusema kuwa hakuna timu inayobebwa na TFF bali kila timu imepangiwa kulingana na mzunguko wake.

Hayo yamesemwa mapema leo septemba 12, 2016 na afisa habari wa TFF, Alfredy Mapunda akifanya mahojiano na dar24.com katika ofisi za shirikisho hilo zilizopo jiijni Dar es salaam na kuongeza kuwa malalamiko yanayotolewa na baadhi ya timu kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwamba TFF inapendelea  baadhi ya vilabu vinavyoshiriki ligi kuu kuwa siyo ya kweli, ni uzushi tu kwani TFF ni mlezi wa mpira hapa nchini na ni wajibu wake kusimamia vilabu vyote.

Aidha Mapunda  aliongeza kuwa suala la Azam FC la kuutumia uwanja wake siku ya mechi yake dhidi ya simba amesema wameshalimaliza na mchezo huo utachezwa katika uwanja wa uhuru na si Azam Complex kama ilivyodaiwa hapo awali.

Serengeti Boys Yaifunga Dynamo, Kutua Usiku Wa Manane
Serikali Yashauliwa Kusimamia Miradi Ili Kuhakikisha Malengo Yanafikiwa