Mwimbaji wa Nigeria, Timaya ameuanza mwaka kwa kuachia video ya wimbo wa kwanza kutoka kwenye albam yake mpya ya ‘Chulo Vibe’, wimbo ambao ameubatiza jina la ‘Balance’.

Balance ni ngoma ya kwanza kutoka kwenye Extended Play ya ‘Chulo Vibe’ ambayo wachambuzi wanaisifu kwa namna alivyocheza na melodies pamoja na vibwagizo vinavyoshika umakini wa msikilizaji kwa haraka, ni mradi wake wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano.

‘Balance’ imepikwa na Orbeat, mtayarishaji ambaye ni swahiba wake wa muda mrefu. Video imeongozwa na Unlimited LA.

Enjoy:

Wafanyabiashara Tarime wapokea mradi wa bil. 8
Siri ya Mpoto kutembea peku yavuja, amtaja Ruge nyuma ya pazia

Comments

comments