Mtangazaji na mwandaaji wa vipindi vya runinga, na mchambuzi wa filamu hapa nchini, Zamaradi Mketema mara baada ya kutambulisha ujio wa filamu mpya ya Cop’s Enemy iliyowashirikisha wasanii wakubwa na maarufu Afrika akiwemo Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na Van Vicker ameachia ‘trailer’ ya filamu hiyo akiwataka watanzania kutoa sapoti kubwa kwa kuitazama filamu hiyo mara baada ya kuachiwa hewani.

Filamu hiyo iliyogharimu takribani pesa za kitanzania milioni 200, na kutayarishwa kwa zaidi ya miaka miwili, itaonyeshwa katika mtandao maalumu wa kurusha filamu wa Netflix unaotazamwa na zaidi ya watu milioni 139 duniani kote.

Filamu ya Cop’s Enemy imetayarishwa wahariri kutoka Australia kwa kushirikiana na meneja wa msanii Wema Sepetu Neema Ndepanya ambapo inatoa nafasi kwa watu wenye rika zote kupata fursa ya kutazama filamu hiyo kutokana na maudhui yake, kama hujabahatika kutazama kionjo ”Traller ya Filamu hiyo bonyeza link hapa chini kutazama.

Zari ataja sifa ya mwanaume anayemtaka, 'Diamond hana pesa'
Live: Kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini

Comments

comments