Nchini China, kaunti ya Taiwan Treni ya Puyuma Express 6432 imepata ajali mbaya mara baada ya mabehewa yake yote nane kutoka katika njia yake kaskazini-mashariki mwa Taiwan na kupata ajali ilipokuwa inakaribia stesheni ya Xinma karibu na mji wa Su’ao.

Treni hiyo iliyokuwa imebeba abiria 366 ikifanya safari zake kati ya Taipei na Kaunti ya Taitung imepoteza maisha ya abiria 18 huku wengine 170 wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Hata hivyo Mamlaka ya reli imesema inafanyia uchunguzi ajali hiyo iliyotokea katika kaunti ya Yilan siku ya Jumapili na tayari imewatoa watu wote waliokuwa kwenye treni hiyo

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya reli ya Taiwan, Lu Chieh-shen, ameviambia vyombo vya habari kuwa treni hiyo ilikuwa na miaka sita na ilikuwa na hali nzuri kabla ya ajali kutokea.

Haijajulikana mara moja sababu ya treni kutoka nje ya reli yake, lakini mashahidi walisema walisikia kelele kubwa, cheche na moshi. Vikosi vya zima moto vinasaidia majeruhi na wizara ya ulinzi imesema inapeleka wanajeshi 120 kusaidia jitihada za uokoaji.

Mashuhuda walilazimika kuvunja vioo ili kutoka nje ya mabehewa, na baadhi ya waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.

Mwanahabari kutoka shirika la habari la Ufaransa aliyekuwa kwenye eneo la tukio amesema miili imekuwa ikiondolewa kutoka kwenye mabehewa yaliyoharibika.

Kiongozi wa Taiwan,Tsai Ing-wen, amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa ni tukio baya sana. Taiwan ina mtandao mkubwa sana wa usafirishaji wa treni, na zaidi ya nusu milioni ya abiria husafiri kwa treni kila siku.

Trump azidi kuivimbia Urusi
Video: Sh 1 bilioni kutekwa Mo Dewji zakosa mtu, Mwacheni Mo apumzike - Baba