Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limeishauri Serikali kuwezesha bodi ya mishahara kukutana na kufanya utafiti utakaowezesha kupangwa kiwango halisi cha kima cha mshahara.

Hayo yamesemwa jijini Mbeya na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Dkt. Yahaya Msigwa wakati wa sherehe ya maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi, ambapo amesema kuwa wafanyakazi ni wachangiaji wakubwa wa safari ya kuelekea uchumi wa viwanda.

Amesema kuwa wanatambua kuwa kwenye baadhi ya mashirika ya umma miundo ya utumishi haijapitishwa na mamlaka husika, jambo ambalo linazuia nyongeza ya mishahara kila mwaka.

”Tunaiomba serikali miundo hii ipitishwe ili ianze kutumika ili kila mwaka mishahara iweze kuwa inaongezeka kwa watumishi wa sehemu husika ili wafanyakazi waweze kuboresha maisha yao,”amesema Dkt. Msigwa

Aidha, amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuweza kusikiliza ombili la kuweza kupunguziwa kodi ya mshahara, ingawa amesema kuwa idadi ya wafanyakazi wanaonufaika na punguzo hilo ni wachache.

Akihutubia katika maadhimisho hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kuhusu ahadi yake ya kuwaongeza mishahara watumishi wa umma, amesema kuwa muda wake wa uongozi haujaisha hivyo, wasiwe na wasiwasi.

 

 

Mwanafunzi mbaroni kwa kujiteka
Serikali kurasimisha ajira ya kuokota Makopo