Baraza la Vijana la Chadema BAVICHA limeitaka Serikali kutoa majibu ya kueleweka kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada huku ikihusishwa na deni inalodaiwa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa kashfa ya kukamatwa kwa ndege hiyo ni lazima itolewe taarifa kamili.

“Hata kama wakitukamata Chadema wote watuweke rumande, hatutakaa kimya acha waendelee kutukamata sisi wapinzani, kwa hiyo sisi tuanataka majibu ya hoja yetu ya kuhusu ndege ya yetu,”amesema Katambi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kuna mtu ambaye ametishia uhai wa mwanasheria mkuu wa chadema, Tundu Lissu kuwa anaomba kupewa ruhusa ya kumshughulikia mwanasheria huyo.

Video: Wabunge wapya wa CUF wataapishwa kama ilivyopangwa- Ndugai
Maya Yoshida Anogewa St Mary's Stadium