Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ishirikiane na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali na wataalamu kutoka chuo kikuu cha ardhi kuhakiki eneo lenye ukubwa wa hekta 475,052 lililoripotiwa na Tume hiyo kuwa linafaa kwa kilimo cha Umwagiaji nchini.

Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam ili kuongea na watumishi, ambapo aliwataka wao kama Tume washiriki kwanza kuhakiki eneo hilo na kuweza kutoa taarifa za uhakika.

“Mnaweza kushirikiana na ofisi za kanda na halmashauri ili kuweza kurahisisha kufanyika kwa kazi hii ,kwenye kilimo ni vyema tukaendana mambo yote matatu, kilimo cha kutegemea maji ya mvua, kilimo cha kutegemea maji ya ardhini na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji cha kutumia miundombinu, kilimo ambacho kitatuhakikishia uhakika wa chakula kwani ni kilimo ambacho mkulima analima zaidi ya mara moja kwa mwaka,”amesema Mgumba

Yaya Toure hatarini kuvunja mkataba Olympiakos
Saudia yapingana na CIA, yadai Mwanamfalme hakuhusika na mauaji ya Khashoggi