Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imeamua kuhakikisha Tanzania inapata umeme wa uhakiki na kuachana na umeme wa matapeli kwani Serikali imeamua kujenga nchi kwa viwanda hivyo lazima umeme uwepo wa kutosha na uhakika.

Rais Magufuli amesema nia yake ni kuhakikisha mawazo ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya kuzalisha umeme kutoka maporomoko ya mto Rufiji, yanatekelezwa haraka iwezekanavyo.

Rais Magufuli amesema hayo baada ya kukutana na timu ya wataalamu wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme iliyotumwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Tanzania.

“Sasa hivi nchi yetu inazalisha megawatts 1,450 tu, lakini Stiegler’s Gorge itatuzalishia megawatts 2,100 umeme huo ni mwingi na utatusaidia katika viwanda, hivyo Serikali tumeamua kutekeleza mradi huu.

“Najua kutaanza kutokea vipingamizi mbalimbali, lakini naomba Watanzania tuwe na sauti moja, eneo litakalotumia ni Kilometa za mraba 1,350 ambalo ni sawa na asilimia 3 tu ya eneo lote la hifadhi ya Selous yenye ukubwa wa Kilometa za mraba 45,000” amesema Rais Magufuli

Kiba adai kusingiziwa mtoto na mwanamke wa kimombasa, ahoji majibu ya DNA
Thomas Lemar Kumrithi Alexis Sanchez