Mkuu wa Wilaya ya kinondoni, Ally Hapi  amesema wilaya yake imejipanga vizuri kuelekea katika kilele cha kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es salaam kwa kukagua mifumo ya maji katika jiji ilikuhakikisha miti itakayopandwa isikauke kwa kukosa maji katika barabara zote za jiji.

Hapi amesema hayo alipokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kukagua maandalizi ya siku ya upandaji miti maarufu kama ‘Mti wangu’. Hapi amesema katika maandalizi hayo tayari wameshatoboa baadhi ya barabara ili kupitishia mabomba ya maji  kutoka katika barabara za Salender bridge mpaka Moroco, Kigogo mpaka Magomeni,  barabara ya  Mwenge mpaka Milimani city.

”Tumeelekeza makampuni yote yaliyopo pembeni mwa barabara kutunza maeneo yao na kuyapanda miti ili kuhakikisha kampeni ya kupamda miti inafanikiwa” – Hapi.

Waziri Mkuu kuhamia Dodoma kesho
Video: Makonda afanya ziara ya kukagua maeneo yatakayo pandwa miti Oktoba mosi