Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro kukamatwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya kuhojiwa ambapo amesema hapakuwa na sababu yeyote ya kumkamata.

Lema amesema kuwa Meya wa jiji hilo alipata mwaliko kutoka kwa umoja wa wamiliki wa shule binafsi jijini Arusha kwenda kutoa rambirambi katika Shule ya Lucky Vincent kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32 waalimu wawili na dereva.

“Nimesikitishwa sana baada ya kupokea taarifa hizo, lakini bado najiuliza hivi hata kwenda kutoa rambirambi na kwenyewe mpaka tuombe kibali,”amesema Lema

Amuua mama yake ‘siku ya mama duniani’, azurura mtaani na kichwa chake
Muhimbili kuboresha maslahi ya wauguzi

Comments

comments