Serikali imedhamiria kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo ambapo Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Sekta ya Kilimo (ASLMs) na wadau wa kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya pili (Agricultural Sector Development Programme Phase Two-ASDPII).
 
Katika utekelezaji wa ASDP II serikali imelenga kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo mazao, mifugo na uvuvi ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha na usalama wa chakula na lishe.
 
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania.
 
Amesema kuwa utekelezaji wa lengo hilo ni kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula, kuimarisha uchumi, kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda na kuongeza ajira.
 
“Tumeanza na mbolea ambapo kwasasa inaagizwa kwa pamoja na tumeondoa kodi na tozo nyingi katika mbolea ili ipatikane kwa bei nafuu. Kwasasa changamoto kubwa imebaki kuwa gharama kubwa ya usafirishaji hasa kwa maeneo ambayo hakuna usafiri wa reli ambapo Serikali bado inalifanyia kazi suala hili,” amesema Hasunga

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 27, 2018
Takukuru yamburuza mahakamani mtumishi wa DAWASA