Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) mkoa wa Arusha, Zubery Mwinyi amesema kuwa wanamtambua Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba.

Ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa wanamtambua Prof. Lipumba kuwa ni Mwenyekiti Taifa, huku akisema Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif amesimamishwa kwa muda.

Aidha, katika hatua nyingine Zubery amesema kuwa kwasasa hakuna Umoja wa Katiba Wananchi (UKAWA) mkoani humo hivyo watasimamisha wagombea katika chaguzi zote ndogo ndogo za marudio.

“Kwanza nianze kwa kusema kwamba CUF Arusha tunamtambua Mwenyekiti wetu Prof. Lipumba, lakini tunachojua kingine Katibu wetu amesimamishwa kwa muda, lakini ikumbukwe tu kwamba Arusha hakuna Ukawa, ndio maana tumesimamisha wagombea katika Kata zote zilizorudiwa uchaguzi,”amesema Mwinyi

Video: Ndugu wasusa kumzika aliyefia mikononi mwa polisi, kamanda afunguka
Askari waliowapiga wanahabari kutiwa mbaroni