Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori amesema kuwa katika utendaji kazi wake anasimamia taratibu kwa usahihi na kwa kufuata sheria, hivyo mtu yeyote anayevunja sheria huchukuliwa hatua bila kujali anatoka chama gani.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa sheria ni msumeno hukata pande zote mbili bila kujali ni nani aliyetenda kosa.

Aidha, amesema kuwa mtu yeyote anayesimamia sheria mambo huwa yanaenda vizuri hivyo hakuna changamoto kubwa katika suala hilo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ikumbukwe kuwa serikali iliyopo madarakani inatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo hata Halmashauri inayoongozwa na upinzani bado inatekeleza Ilani ya CCM.

Chadema yazidi kuyeyuka Iringa, madiwani 7 wajiengua wakimtuhumu Mch. Msingwa
Kimenuka Kagera Sugar, Mexime atoa tamko

Comments

comments