Shule maarufu ya mfumo wa kiingereza ya Tusiime iliyopo Tabata Segerea jijini Dar es Salaama imetozwa faini ya shilingi milioni kumi kwa kukiuka sheria ya mazingira ya 2004, kwa kutiririsha majitaka nje ya mfumo wa DAWASCO na kuhatarisha maisha ya mazingira na viumbe hai.

Faini hiyo imetolewa leo Oktoba 6, 2016 na Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki kutoka NEMC, Jaffar  Chimgege katika Ziara ya Naibu Waziri wa Mazingira, Luhaga Mpina ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es Salaam, ambapo wamefika shuleni hapo na kubaini kuwepo kwa utiririshaji wa maji taka yasiyotibiwa katika mazingira na maeneo ya wakazi majirani na shule hiyo. Hivyo ameutaka uongozi wa shule hiyo kutafuta mfumo mbadala  na wenye kukidhi viwango ya utiririshaji wa maji hayo pamoja na kujengea mitaro inayotoa maji taka shuleni hapo.

“Hatutakubali wawekezaji wenye mashule, viwanda, hospitali na hotel kuchafua mazingira kwa kutiirisha maji taka  yasiyothibitishwa kwenye mazingira”. – Naibu Waziri Mpina. Bofya hapa kuazama video

 

 

DC Staki ashiriki shughuli za kijamii
Video: Waliovamia shule kuondolewa