Taasisi ya Kupambana na Kuzuia na Rushwa (TAKUKURU) leo Juni 19, 2017 imewafikisha mahakamani wafanyabiashara wawili James Rugemalira na Harbinde Seth watuhumiwa wawili wa kesi za ESCROW na IPTL.

Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo wamesomewa mashtaka sita yanayowakabili likiwemo la uhujumu uchumi.

Mahakama hiyo imesema upelelezi bado unaendelea na haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa watuhumiwa hivyo wamerudishwa rumande.

Video: Waziri Mkuu azindua Kamusi Kuu ya Kiswahili
Zitto ampongeza Rais Magufuli, "Umeitendea nchi haki, hongera sana"

Comments

comments