Rais wa Marekani, Donald Trump jana tarehe 27 Agosti, 2018 alifanya mkutano na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya ‘White House’ iliyoko mjini Washington, huku masuala ya usalama, ulinzi na biashara yakiteka mkutano huo.

Marais hao kwa pamoja walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika kupambana na ugaidi nchini Kenya pamoja na kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya mataifa hayo mawili.

Sambamba na makubaliano hayo, Rais Trump na Kenyetta walisaini mitaba mbalimbali yenye jumla ya thamani ya dola za kimarekani milioni 900.

Rais Kenyatta anakuwa kiongozi wa tatu kutoka mataifa yaliyoko Kusini mwa Jangwa la Sahara kukaribishwa Ikulu ya White House sambamba na kufanya mazungumzo na Rais Trump.

Ommy Dimpoz: 'Nilitia saini kufa au kupona'
Video: Makonda amalizwa, Upinzani watabiriwa kufa