Idara ya Uhamiaji imesema kuwa hati za kusafiria za zamani zitaendelea kutumika mpaka ifikapo Januari 2020, hivyo watumiaji hawapaswi kuwa na wasi wasi wowote.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda alipokuwa akizumgumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kwasasa zitaendelea kutumika sambamba na zile za Kielektroniki.

Amesema kuwa kwa wale ambao hati zao zimeisha muda na wanataka kubadilisha watashauriwa kuchukua hati za kusafiria za Kielektroniki.

Hata hivyo, ameongeza kuwa mfumo huo ni mzuri hivyo, watumiaji hawapaswi kuwa na wasiwasi wowote kuhusu matumizi yake.

Video: Viongozi wa dini liombeeni Taifa - Makonda
Video: CUF, Chadema watunishiana misuli Kinondoni